January 8, 2020


NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa watapambana kufanya vizuri kwenye Kombe la Mapinduzi baada ya kutinga hatua ya nusu fainali.

Bocco amesema kuwa wanatambua kazi kubwa waliyonayo ni kutafuta ushindi jambo ambalo watalifanya siku zote.

Kwenye ushindi wa mabao 3-1 aliyopata Simba mbele ya Zimamoto, Bocco naye alitupia bao moja huku mengine yakifungwa na Sharaf pamoja na Ibrahim Ajibu.
 
"Mashabiki wanahitaji kuona timu inapata matokeo chanya, tupo vizuri na tunaendelea kupambana kwa ajili ya kufikia malengo na mafanikio, tunaamini tutapata kile ambacho tunakihitaji.

"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo tutakachofanya ni kujituma ndani ya uwanja," amesema Bocco.
Siba itamenyana na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa, Januari 10uwanja wa Gombani

5 COMMENTS:

  1. Apigwe azam 3 tukutane na huyo kandambili aka vyura wa jangwani na wao wale 4g ila kipa awe kakolanya

    ReplyDelete
  2. Sipendi maneno maneno mpira ni vitendo

    ReplyDelete
  3. Jamani mechi ya yanga na mtibwa saa ngap na simba na azam saa ngap

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic