PIERRE-Emerick Aubameyang amesema kuwa anaipenda klabu yake ya Arsenal na hana mpango wa kutimka kwa sasa.
Aubameyang ambaye ni nahodha wa kikosi hicho ameyasema hayo baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba anaweza kujiunga na klabu ya Barcelona.
Ilielezwa kuwa kutokana na matokeo mabovu ya timu yake hivi karibuni alikuwa anataka kuondoka ndani ya timu hiyo.
"Sina mpango wa kuondoka kwa sasa ndani ya timu yangu ya Arsenal, ninaipenda na nitaendelea kuwepo hapa hivyo sifikirii kuondoka kwa sasa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment