KOMBE la Mapinduzi
linazidi kuchanja mbunga taratibu kueneleka kumtafuta bingwa wa mwaka 2020.
Tayari timu zimeanza kujiengua ambapo tangulianze kumtafuta mbabe wake huko visiwani Zanzibar, Januari, 6,2020 tayari wengine wameshajiengua.
Azam FC ilianza kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali kwa kushinda mbele ya Mlandege kwa bao 1-0 kisha Mtibwa Sugar ilitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa penalti 4-1 mbele ya Chipukizi baada ya dakika tisini ngoma kuwa sare ya bao 1-1.
Kwa upande wa Yanga wao wameshamaliza kete zao baada ya kuanza robo fainali vema mbele ya Jamhuri kwa ushindi wa mabao 2-0 kabla ya kutolewa na Mtibwa Sugar kwa changamoto ya penalti 4-2 baada ya dakika tisini kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1.
Ni aina ya michuano
ambayo ipo katikati ya Ligi Jambo linalofanya Ligi isimame kwa muda kulingana
na shughuli nzima ya michuano hii ambayo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja kwa baadhi ya timu ambazo zinashiriki.
Timu zinazoshiriki zilikuwa nane safari hii na zote ni za Tanzania tofauti na zamani ambapo kulikuwa na
waalikwa ambao walikuwa wanakuja kunogesha mashindano haya ambayo yana heshima
yake.
Ukiachana na kutokuwa
kwenye kalenda ya Fifa bado ni miongoni mwa mashindano ambayo yamekuwa yakikuza
na kukomaza viwango vya wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi ya kuonyesha
kile ambacho wanacho.
Mashindano yanatoa fursa
ya kutambua uwezo wa wachezaji husika wa timu moja na kurahisisha kazi kwa
mwalimu katika kupanga kikosi kazi ambacho atakitumia wakati wa mashindano
mengine nje ya Mapindizi yenyewe ambayo hayachukui muda mrefu.
Kutokana na sababu
hiyo wengi wamekuwa wakiyapuuzia na kuchukulia ni mashindano ya kawaida ila
ukweli ni kwamba si kama ambavyo wanafikiria yana umuhimu wake kuwepo ndani ya
ardhi ya visiwani Zanzibar.
Miongoni mwa sababu zinazofanya
yawe na umuhimu kwa kuwa inafanya muunganiko uzidi kuwa imara kutokana na
kushirikiana katika masuala ya kitaifa na kutufanya tuzidi kuwa na umoja.
Sisi site ni ndugu na
tunapozidi kuwa karibu tunaongeza ukaribu wetu na undugu wetu kwa nchi ambayo
inasifika kwa amani na upendo itazidisha kuujenga upendo kwa ndugu na wengine
ambao bado wapo kwenye muungano kwa muda mrefu.
Wachezaji wote
ninapenda kuwaambia kwamba ishu ya Mapinduzi sio muda wa kucheza kwa kukomoana
hii sio sawa ni vema mpira wa kiungwana ukachezwa na kila mmoja akafanya vema kwa
kipaji alichopewa na Mungu.
Kazi ya usalama wenu
mkiwa ndani ya Uwanja ipo mikononi mwa wachezaji ni muhimu kulizingatia hilo na
kulifanyia kazi kwa wakati kabla ya kuanza kuendelea kutafutiana visasi visivyo
na maana.
Ikumbukwe kuwa
mchezaji akipata majeruhi wakati huu itamfanya akose mechi kutokana na kuwa bize
kutibu majeraha yake hili jambo linaumiza hasa ukizingatia ni ndani ya wiki
moja Ligi itaendelea.
Ninachokiona ni kwamba
mlinzi wa kwanza kwenye haya mashindano ni mchezaji. Jukumu kubwa la kucheza kwa
umakini bila kusahau kucheza soka linaloeleweka uwanjani.
Uwepo wa mashabiki
ambao watatupa keki ya uwanjani ni muhimu wakajilinda wenyewe na kufanya kazi
ya kutoa burudani kwa mashabiki ambao wameshaanza kutoka makwao na wengine
wakijiandaa kuja kuitazama.
Kila timu isikubali
kuonyesha ubabe ila kwa namna makundi yalivyo na ushindani ulivyo ni imani
yangu kwamba kila mchezaji ana kazi ya kuwa mlinzi wa mchezaji mwenzake ndani
ya uwanja ili kumfanya awe salama muda wote.
Mgawanyo wa makundi
pia mawili unatoa picha kwamba ushindani utakuwa mkubwa na rai yangu kwa wachezaji
katika hali ya kawaida itawafanya wawe bora.
Mtindo wa kuchezeana
rafu ndani ya mechi na kisha kutafuta sababu na kuomba msamaha hii haileti afya
kwenye kazi ya soka letu kikubwa wachezaji wanatakiwa kuwa makini wawapo ndani
ya Uwanja.
.
Mpira wa miguu una
purukushani kwa sasa ndani ya uwanja ila haitoi fursa kwa wachezaji kucheza
rafu ambazo hazina maana kwa wachezaji itawaumiza wachezaji wengine.
Ulinzi wa mchezaji na
afya ya mchezaji ni muungano mzuri utakaofanya mapinduzi bora kwenye soka letu
la Bongo kiujumla kwani amani itatawala.
Itakuwa furaha kuona
namna mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wakikutana na ushindani
na wakatoa burudani bila wachezaji kuchezeana rafu sizizo na maana itapendeza.
Kila kitu kinawezekana
ni suala la kukubali na kujituma kwa wachezaji wetu huku wakiongeza umakini
maradufu wawapo ndani ya uwanja kutimiza majukumu yao ipasavyo. Nina imani
hawatatuangusha katika hili.
Mashabiki kazi yenu ni
moja kuleta shangwe muda wote na sio kusubiri chenga ama goli hapana hii si
nzuri ni mwaka mpya na habari nyingine zinapaswa zifanywe kwa utofauti.
Shangilia ya mashabiki
itaongeza utamu wa Mapinduzi na kila mmoja akitimiza jukumu lake itafanya kazi
kuwa bora na kila mmoja kufurahi kupata burudani, kila la kheri wachezaji
pamoja na mashabiki tunahitaji kuona bingwa bora anapatikana.
Timu shiriki
zinapaswa zionyeshwe maana halisi ya kushindana kwa kutoa burudani na kucheza
kwa juhudi bila kujali aina ya timu ambazo wanakutana nazo.
Wachezaji
wengi huwa wanatatzio la kudharau mechi jambo ambalo halipaswi kutokea kwenye maisha
ya soka letu kwani dakika tisini ndizo zenye majibu sahihi ya kile
unachokitafuta.
0 COMMENTS:
Post a Comment