KWA sasa kila
mmoja anacho kile ambacho alikuwa akijenga picha kwa muda wa miezi kadhaa nyuma
ambapo kila mmoja alikuwa anavutia upande wake kwa kile alichoamini ni bora.
Simba na Yanga hapa
ndio nazungumzia baada ya kucheza mchezo wao wa kwanza kwa msimu wa 2019/20,
January 4,2020, balaa lilikuwa ni kubwa uwanjani na mwisho wa siku mbabe hakuna
kati yao kwa sasa zile tambo zimepungua.
Leo sitapenda
kuzungumzia matokeo kwani kila mmoja anatambua kuwa ilikuwa sare ya kufungana
mabao 2-2 pale uwanja wa Taifa kwa hilo inatosha kujua kwamba hizi timu
zinajuana na zina historia kwa muda mrefu.
Kidogo tu naweza
kugusia kwa kuwapa pongezi wachezaji wa Yanga Kwa kuonyesha ukomavu wao mwanzo
mwisho bila kukata tamaa licha ya kuwa nyuma kwa kufungwa mabao mawili na watani
zao Simba ambao walipania kushinda.
Ukweli ni kwamba
kilichowapa nguvu ya kupambana Yanga ni ile nguvu waliyokuwa nayo na sapoti
kutoka kwa mashabiki walionyesha nidhamu ya soka kwa kutulia na kuwaheshimu
wapinzani wao.
Kwa upande wa Simba
hili linapaswa liwe fundisho hawapaswi kudharau timu pinzani hata wakiwa mbele
kwa mabao matano kabla mpira haujaisha kwani kilichotokea baada ya kufungwa bao
moja walipoteza matumaini na kuanza kucheza bila kujali wanafanya nini.
Walisahau majukumu yao
uwanjani na wakaruhusu kuanza kumtafuta mchawi nani ndani ya uwanja wakati
mpira unaendelea na hakuna ambaye alikuwa anajali jambo hili hiki kiliwavuruga
Simba .
Inaonesha kuwa ndani
ya Simba kwa sasa kila mchezaji ni mkubwa kuliko mwenzake hakuna anayetaka
kumsikiliza mtu mwingine zaidi ya kufanya kile anachokiamini hili halipo sawa
na kama ni utamaduni mpya unapoteza ladha na asili ya Simba na mpira kiujumla.
Mpira hautoi muda wa
kuanza kumtafuta mchawi wakati bado kuna muda wa kupambana badala yake unatoa
muda wa kurekebisha makosa na kuongeza mshikamano mwanzo mwisho.
Nimeamua niligusie kidogo
kwani likifumbiwa macho kwa sasa litakua tatizo kubwa ambalo litafuta mazuri
yote ya wachezaji ndani ya timu pamoja na uongozi kiujumla.
Pia mashabiki kwa
kujitokeza uwanjani nawapa pongezi wote si wa Simba wala Yanga uwanja
ulipendeza na hamasa ilionekana mwanzo mwisho ndani na nje ya uwanja wa Taifa.
Hiki ndicho ambacho
kinatakiwa kifanyike siku zote na kuendelea kuona ni namna gani mambo yanaweza
kubadilika ndani ya mwaka 2020 kwenye suala la ushangiliaji na kujitokeza
uwanjani.
Simba walikuwa
wanyonge baada ya matokeo na hii ilitokana na kujiamini kupiga kiasi wakiwa
ndani ya uwanja kwa hili linapaswa lifanyiwe kazi pia na benchi la ufundi
pamoja na uongozi kiujumla ujue ni namna gani unaweza kurudisha ari ya timu.
Kwa mwenendo walionao
kwa sasa endapo wataendelea namna hii na kujiachia wakiwa uwanjani mambo
yatakuwa tofauti na vile ambavyo wanafikiria kwani wachezaji walionyesha kukubali matokeo waliyoyapata.
Morali ya timu
inapaswa ijengwe upya na iishi muda wote ndani ya dakika tisini mpaka mwamuzi
atakaposema sasa inatosha na kupuliza kipyenga chake cha mwisho na sio kabla
timu inapoteza ushirikiano.
Yanga nao wanakazi ya
kufanya licha ya kuonekana wao wamekuwa wababe kurudisha mabao yao wasisahau
kwamba ligi bado haijakamilika mambo yanaendelea.
Rai yangu kwa
mashabiki siku zote wanapokwenda uwanjani wasiwe na matokeo yao mfukoni
litawakosesha raha siku zote bali wanapaswa watambue kuwa kazi ya matokeo ni
ndani ya Uwanja kwa wachezaji wenyewe.
Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) linapaswa litazame namna bora ya kuwavuta mashabiki kwenda
uwanjani kuzipa sapoti timu zao na kuona namna gani zinafikia malengo ya
kuongeza hamasa kwa mashabiki.
Ilivyokuwa Simba na
Yanga ikipewa promo basi uwe pia hata wakati KMC itacheza na Ndanda kwa kutoa
taarifa mapema na kuangalia mambo ambayo yatawaweka karibu wachezaji.
Sapoti na nguvu kubwa
kwa mashabiki na TFF inapaswa iendelee siku zote bila kufikiria ni timu ipi
ambayo inacheza kwenye mechi zao za ligi pamoja na za mashindano mengine.
Hali hii ya kuzipa
sapoti timu zetu isiishie kwenye ligi tu inapaswa izidi kuendelea muda wote
katika kazi na kuendelea kushuhudia ligi ikizidi kupamba moto.
Mashabiki ni muhimu
kuendelea kutoa sapoti kwa timu zote kwa kuwa mpira unahitaji sapoti na kuna
namna gani wachezaji watafanya kazi zao ndani ya uwanja.
Kwa wachezaji pia iwe
somo kujifunza kupitia makosa na kufanya kazi kwa juhudi ndani ya uwanja bila
kujali aina ya timu ambayo unacheza nayo.
Jana vipi kuna alieenda na matokeo uwanjani huko Zanzibar?
ReplyDeleteDUH!!!
ReplyDeleteAnonymousJanuary 10, 2020 at 2:01 PM
ReplyDeleteYanga walijua watapenya kwa urahisi.Wakijua kwamba wanaweza kupambana na Simba waliamua kupumzisha wachezaji wa kikosi cha kwanza..Yondani aliingia toka benchi baada ya kuwa tayari wamefunga.Lamine aliendelea kubaki benchi...Haruna na Sibomana hawakuwepo.Golini alikaa kipa namba tatu.Lengo kikosi cha kwanza kiwe fiti ili kucheza mchezo wa nguvu na rafu kama ilivyokuwa kwa Prison na Simba.Wakatunguliwa sekunde ya mwisho gemu plan ikaanza upya.Kikawa kisingizio toka kwa Nungaz eti wamekuja kushindana sio kushinda na kuwa hawakulitaka kombe lisije waumizia wachezaji!Sasa sijui kombe gani wana uhakika nalo...la FA au la Premium league