UONGOZI wa Singida United umesema kuwa uwepo wa wakongwe ndani ya timu hiyo umeanza kuwapa matokeo ya kile ambacho walikuwa wamekikosa kwa muda mrefu.
Singida United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ramadhan Nswazurimo haina matokeo chanya kwenye mechi zake za ligi kwani kwenye mechi 16 ilizocheza imeshinda mechi mbili pekee ya kwanza ilikuwa mbele ya Mbeya City kwa ushindi wa bao 1-0 na jana, Januari 11 ilishinda mechi yake ya pili kwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa wanajivunia kuanza kuyaona matokeo kwa wachezaji wao.
"Tunapita katika kipindi kigumu kwa sasa hasa kwa upande wa matokeo, tunachokifanya ni kuona namna gani tutaweza kurejea kwenye ubora ila hawa wakongwe naona wanatupa kile ambacho tulikosa kwa muda mrefu.
"Kikubwa mashabiki wazidi kutupa sapoti kwani kwa sasa tumerejea kwenye uwanja wetu wa nyumbani na hii itatoa fursa kwao kuona ile burudani waliyoikosa kwa muda mrefu," amesema.
Miongoni mwa wakongwe ndani ya Singida United ni pamoja na Haruna Moshi, 'Boban', Athuman Idd, 'Chuji' ambao wote wamepewa kandarasi ya miezi sita.
0 COMMENTS:
Post a Comment