OBREY Chirwa, mshambuliaji wa Azam FC ameipekeka timu yake kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Mlandege.
Chirwa alifunga bao la ushindi dakika ya 59 kwenye mchezo huo uliochezwa visiwani Zanzibar akimalizia pasi ya Joseph Mahundi kwa kichwa.
Chirwa amesema kuwa anajiskia faraka kuipa ushindi timu yake ni zawadi kwa mashabiki wote wa Zanzibar.
"Najiskia faraja kuona namna gani vile timu inapata matokeo chanya, ni furaha kwa timu na uongozi kiujula," amesema.
Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe hili walitwaa 2019 baada ya kuifunga Simba mabao 2-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment