January 10, 2020


Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwassa, amesema kuwa wachezaji waliosajiliwa ndani ya Yanga ikiwa ni pamoja na Yikpe Gnamien na Haruna Niyonzima ni watu wa kazi na watadhihirisha hilo kwa vitendo.

Mkwasa alisema kuwa wachezaji hao bado hawajawa na muunganiko mzuri ndani ya kikosi kutokana na kutokaa muda mrefu na timu.

“Ukimzungumzia Niyonzima yeye anabebwa na uzoefu alionao pamoja na kuitambua Ligi ya Tanzania ila kwa huyu Yikpe na wenzake ambao ni wapya taratibu watazoea mazingira na watafanya kazi.

“Imani yangu ni kuona kwamba kila mmoja anaonyesha uwezo akiwa uwanjani kwa muda ambao nimekaa nao tayari nimegundua kitu cha kipekee kwao jambo moja tu nawaambia mashabiki wanapaswa watulie wasubiri matokeo, hawa ni watu wa kazi na wataonyesha kazi yao,” alisema Mkwasa.

Yanga kwa sasa ipo Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi, kete yake ya kwanza ilikuwa jana usiku saa mbili mbele ya Jamhuri Uwanja wa Amaan.

1 COMMENTS:

  1. Hii blog imekua yakisenge sana sasa mnaandika ujinga gani hapa??yanga ameshacheza mpaka nusu fainali leo mnatuambia eti ndio ametupia kete yake ya kwanza mikundu nyie hamko sawa fungeni blog kama imewashinda acheni habari zakisenge tumewachoka mjue.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic