RAMADHAN Kabwili, mlinda mlango namba tatu wa Yanga amesema kuwa leo wameshindwa kupeta mbele ya Mtibwa Sugar kutokana na bahati kutokuwa upande wao.
Kabwili aliweza kuokoa michomo ya hatari leo kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Amaan licha ya kutolewa na Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kabwili amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kukaa langoni kutokana na kutokuwa na muda mwingi langoni ila uzoefu wake na mchezo mbele ya Jamhuri umemsaidia kumrejesha kwenye ubora.
"Nilikuwa nje kwa muda mrefu ila mwisho wa siku nimepata nafasi ya kucheza ndani ya dakika 180 huku kwenye kombe la Mapinduzi.
"Nawapongeza wapinzani wetu Mtibwa Sugar wamecheza vizuri na wameonyesha juhudi kubwa kwa kuifunga timu kubwa yenye presha," amesema.
Kibwana Shomari mfungaji wa bao la kusawazisha leo dakika ya 90 na penalti ya mwisho amesema kuwa wanamsubiri mshindi yeyote yule hawana mashaka katika hilo.
Saleh Ally andika makala ya kuipamba Yanga.
ReplyDeleteYanga ilienda na matokeo mfukoni walijua watashinda hivyo wakapumzisha kikosi kitakacho cheza fainali..Walifurahia sana sare!Endeleeni kufurahia sasa zinawarudia!
ReplyDeleteMpaka sasa juu Ya kukusanya nyota wa bei mbaya kwa kweli inaonesha timu haina msisimko inaonesha wachezaji wanyonge Bila ya hamasa
ReplyDelete