Kichapo cha mabao 3-2 walichokipata Barcelona jana dhidi ya Atletico Madrid kimemkasirisha nahodha wa kikosi hicho, Lionel Messi.
Kwenye mchezo huo wa nusu fainali ya Supercopa uliokuwa na ushindani mkubwa umeshuhudia mabingwa hao watetezi wa La Liga wakitupwa nje jumla.
Licha ya Lionel Messi dakika ya 51 kusawazisha bao la Koke lililofungwa dk ya 46 na Antonio Griezmann dk 62 kupachika bao la kuongoza haikuleta matunda kwao kwani Alvaro Morata dk 81 alisawazisha kwa penalti na Angel Correa dk 86 akakomelea msumari wa ushindi kwa Atletico Madrid.
"Tulicheza bila kufikiria tunahitaji nini, sijapenda kwa namna tulivyofanya, malengo yetu hayajatimia kisa utoto wetu," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment