BEKI wa kati wa Simba, Pascal Wawa, amewaahidi mashabiki wa timu hiyo ushindi dhidi ya wapinzani wao Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Januari 4 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Beki huyo amekuwa na uhakika wa kuanza kwenye kikosi cha Simba sambamba na Erasto Nyoni katika mechi muhimu za timu hiyo tangu asajiliwe na Simba mwaka 2018.
Wawa alisema kuwa malengo yao msimu huu ni kubeba ubingwa wa ligi kuu, lakini ubingwa wao unaambatana na ushindi katika michezo yao pindi watakapokutana na wapinzani wao Yanga.
“Malengo yetu ni kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa ligi, lakini raha ya ubingwa unatakiwa umfunge mpinzani wako wa siku zote, hivyo sisi kama wachezaji tunataka kuhakikisha tunawafunga Yanga katika michezo yote miwili kama zawadi ya ubingwa ambao tunahitaji kuubeba.
“Hayo ndiyo malengo yetu makubwa japo ni ngumu kwa kuwa wapinzani wetu nao wanajipanga kwa hili, hakuna mpinzani ambaye atapenda kupoteza mechi kirahisi lakini kwa upande wetu tumejiandaa kushinda kila mchezo dhidi yao,” alisema beki huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment