NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kupambana kwenye Kombe la Mapinduzi, Visiwani Zanzibar na kuwaomba mashabiki wawape sapoti.
Kombe la Mapinduiz limeanza kutimua vumbi jana na Yanga leo saa mbili usiku itamenyana na timu ya Jamhuri kwenye Uwanja wa Amani.
Jana kikosi kikiwa Zanzibar kilifanya mazoezi kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo huo kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung.
Bingwa mtetezi wa taji hilo la Mapinduzi ni Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment