KOCHA Mkuu wa Biashara United, Francis Baraza ameweka wazi kwamba hawawaogopi wapinzani wao Simba.
Biashara United leo itakuwa na kazi mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.
"Kiukweli
Simba ni timu nzuri lakini siwaogopi kwa kuwa ninapocheza ugenini nina mbinu
zangu ambazo nazitumia jambo linalonifanya nijiamini, hivyo Simba wasitarajie
kupata matokeo kirahisi.
"Ukiangalia
mchezaji mmoja mmoja kwa Simba wana uwezo binafsi na mimi nimeandaa
mbinu zangu ambazo naamini kabisa zitanisaidia kupata ushindi," amesema.
Biashara United ina kazi ya kulipa kisasi mbele ya Simba kwa kuwa mchezo wa kwanza walifungwa mabao 2-0..







0 COMMENTS:
Post a Comment