LUC Eymael,
Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wanashindwa kupata matokeo
mazuri kutokana na ubovu wa viwanja wanavyovitumia wakiwa mkoani.
Yanga
imelazimisha sare kwenye mechi zake nne na kusepa na pointi nne ambapo mbili
ilikuwa Uwanja wa Taifa na mbili ilikuwa viwanja vya mkoani.
Ilianza
mbele ya Mbeya City kwa kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa ikakubali sare tasa
mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Taifa ikafungana bao 1-1 na Polisi Tanzania
Uwanja wa Ushirika, Kilimanjaro na ikamalizia na Coastal Union sare tasa
Mkwakwani Tanga.
“Wachezaji
wangu wanacheza kwenye viwanja vibovu, soka halivutii ndio mana inakuwa ngumu
kupata ushindi kwenye mechi zetu,”.







Na mbili za Dar vipi?
ReplyDeleteVisingizio ambavyo vitakuja kumkosesha heshima kocha, kwani ukweli ni kwamba ukiangalia timu nyingi ndani ya ligi basi Yanga ni timu ndogo changa sana kimuundo na wanahitaji kukua. Kosa la kwanza kubwa Yanga walilolifanya ni kumfukuza mwalimu Zahera. Kosa la pili kubwa ni pale Yanga wanapoilinganisha timu yao na Simba na kuamini kuwa wanastahili matokeo mazuri kama wanayoyapata Simba au kuliko na hii inapelekea presha kubwa kwa wachezaji wakati kiukweli ni kwamba Simba wanashinda mechi zao licha yakuwa na wachezaji wazuri lakini pia pia wazoefu na timu iliyokaa pamoja kwa muda sasa.kwangu mimi hata haya matokeo Yanga wanayoyapata hivi sasa na nafasi waliopo kwenye msimamo wa ligi ni bahati tu kwani wanastahiki kuwa nafasi za mkiani mwa ligi nadhani Yanga huko ndipo watakapomalizia kila ligi ikisonga mbele . Yanga waliitumia mechi ya Simba kuumaminisha umma kuwa wana timu bora lakini lilikuwa ni changa la macho tu. Na Kwa Simba kama kutakuwa hakutafanyika uchunguzi kwa kilichokuwa kinaendelea ndani ya timu yao kwenye mechi kadhaa na kupelekea wachezaji wa Simba kucheza kama wachezaji waliokuwa wakicheza bure basi hujuma hiyo itakuwa inatoka ndani uongozi wenyewe. Kocha wa Simba alikuwa anahujumiwa na kila mtu alikuwa anajua hilo. Labda kutokana na misimamo yake au watu walikuwa wana kocha wao lakini kiukweli kulikuwa na figisu alilotengezewa kocha. Ila yaliopita maovu hayafai kurejewa tena kwani Simba ni taasisi kubwa kunajisiwa na wabinafsi wachache.
ReplyDeleteHA HA HA HA HA HA YANGA BHANA WANAFURAHISHA SANA,ULIONA WAPI MTOTO ALIEVUNJA UNGO/KUBALEHE AKALALA NA WAZAZI KITANDA KIMOJA??LABDA KIKWENU,HATA SIKU MOJA USIILINGANISHE YANGA NA SIMBA MAANA HAIWEZI KUCHUKUA HATA NAFASI YA MAMA KWENYE FAMILIA,POLENI SANA WATANI NA MSIMU UJAO NDIO KABISA MJIPANGE MBONA MNA KAZI.MASIMWAGE POVU.
ReplyDelete