SAFARI ya Ligi Daraja la Kwanza bado inaendelea ambapo kwa sasa timu zimeshaanza kupata picha ya kile ambacho walikuwa wanakifanya kwenye mechi zao za nyuma.
Tunaona kwamba kwa sasa ushindani kwenye Ligi Kuu Bara unazidi kukua kwa kasi jambo linalofanya ligi ivutie na kuwafanya mashabiki wafurahie burudani ya kile wanachokipata.
Kazi kubwa ya kutafuta matokeo uwanjani ipo mikononi wa wachezaji wenyewe wana kazi ya kuwapa burudani mashabiki kwa kucheza kwa juhudi ndani ya uwanja.
Jambo la msingi ambalo linaendelea ni kwamba mashabiki wanajitokeza kwa wingi viwanjani kuwapa sapoti wachezaji wao hili ni la msingi kwani linawapa moyo wachezaji kucheza kwa kujituma.
Kushindwa kupata matokeo mchezo mmoja ama mili kunata nafasi kwa timu iliyoshindwa kujipanga kwa ajili ya mechi zinazofuata kwani ligi ina mechi nyingi kabla ya kukamilisha mzunguko wa pili.
Tunaona kwamba Ligi Daraja la Kwanza inazidi kukata kasi pia ambapo timu zinapambana kupanda daraja ili zishiriki kwenye ligi msimu ujao wa 2020/21 hili ni jambo jema.
Timu zote zinapaswa zitambue kwamba maisha ya Ligi Daraja la Kwanza ni tofauti na huku kwenye ligi ni lazima wakaze buti kabla ya kupanda daraja wasije kurudi walikotoka.
Wengi wamekuwa wakipenda kuishi ndoto zao na kushiriki kwenye ligi huku mipango yao ikiwa ipo palepale ambapo ipo siku zote bila kufanya mabadiliko.
Kuna umuhimu mkubwa kwa timu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kuja na mpango kazi mkubwa utakaowapa matokeo mazuri kwenye ligi ili watakapopanda ligi wasipate tabu..
Kuna umuhimu wa kutazama yale makosa ambayo yanafanyika ndani ya Ligi Daraja la Kwanza ili kuzifanya timu ziwe bora na zenye kuvutia pale zitakapopanda daraja.
Kuna umuhimu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuongeza nguvu pia kwenye kufuatilia masuala yanayowahusu pia hawa wa Ligi Daraja la Kwanza kwani ni msingi wa timu za baadaye.
Tayari tatizo la ukata limeanza kuzikumba baadhi ya timu ambazo hazina udhamini wa uhakika na zinahaha kuendelea kupata fedha.
Achilia mbali zinazohaha zipo ambazo hata uhakika wa kuzipata fedha inakuwa ni tatizo kwao jambo ambalo linaashiria mwendo wa kusuasa kwao katika kutafuta matokeo.
Tumeona hivi karibuni timu ya Njombe Mji ikiomba msaada wa kupewa sapoti pamoja na kupata mdhamini atakayeipa sapoti timu hiyo.
Ikumbukwe pia timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki kwenye Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18 na kwa sasa ipo inahaha kutafuta nafasi ya kushiriki ligi na inapitia kwenye kipindi kigumu.
Hii ni mbaya kwenye kujenga Taifa imara kwenye soka kama msingi wa wachezaji wetu na kule ambako wanatokea wanaishi mazingia ambayo hayana furaha.
Ni wakati wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulitazama hili kwa ukaribu na kuongeza nguvu kubwa kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza nao waishi aina mpya ya maisha kwa kuwa msimu ni mpya.
Kuna uhitaji wa kuboresha viwanja vitakavyotumika na timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kuwa katika ubora na rafiki kwa wachezaji ambao wanacheza.
Timu zimepewa mzigo mzito wa kufanya maandalizi kutokana na kukosa fedha za uendeshaji ni muda wa kuongeza nguvu kwenye uwekezaji wa huku tulikotoka.
Mambo yakiwa imara kwenye timu shiriki ndani ya Ligi Daraja la Kwanza itafanya kupata timu bora ndani ya ligi ambazo zitaleta ushindani wa kweli.
Ligi yetu ya Bongo niweke wazi kwamba ni miongoni mwa ligi ambazo zinafuatiliwa kwa umakini mkubwa na mataifa mengi kitu ambacho kinapaswa kipewe heshima.
Kwenye ligi bora ndani ya Afrika utataja zote utakuwa haujatenda haki usipoitaja ligi ya Bongo ni wakati ambao tunapaswa kuendeleza kile ambacho kipo hasa kwa kutengeneza mazingira mazuri kwa timu zetu.
0 COMMENTS:
Post a Comment