March 6, 2020


CHARLES Mkwasa, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa mbinu iliyowashangaza wengi Januari 4, Uwanja wa Taifa itatumika pia baada ya dakika 90 kwenye mchezo wao watakaocheza Machi 8, Jumapili Uwanja wa Taifa.

Simba ina kumbukumbu ya kupinduliwa meza kibabe na Yanga kwenye mchezo wa kwanza msimu huu ambapo walianza kufunga na Yanga walirudisha mabao mawili ndani ya dakika saba.

Mkwassa amesema: "Ni mchezo mgumu kwetu na tunatambua wapinzani wetu wamejipanga ila nasi tupo tayari kuona tunapata matokeo, mbinu iliyotumika Januari 4 itafanya kazi na mipango mingine mipya,".

Yanga imeshinda mchezo wake wa mwisho kabla ya kumenyana na Simba mbele ya Mbao FC kwa ushindi wa mabao 2-0 huku Simba ikishinda mbele ya Azam FC kwa mabao 3-2 mechi zote zilichezwa Uwanja wa taifa.

Mastaa wao wawili, David Molinga na Patric Sibomana ni wakali wao wa kucheka na nyavu ambapo Sibomana ana mabao matano na Molinga ana mabao nane.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic