BERNARD
Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hakutarajia kumfunga mlinda
mlango wa Simba, Aishi Manula kwenye mchezo wa dabi iliyochezwa Uwanja wa Taifa,
Machi 8.
Kwenye
mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 na mfungaji alikuwa ni Morrison alifunga bao
hilo dakika ya 44 baada ya kuchezewa rafu na Jonas Mkude nje kidogo ya 18.
Ushindi huo
uliifanya Yanga isepe na pointi nne mazima mbele ya Simba msimu huu wa 2019/20
na mabao matatu kwani kwenye mchezo wa kwanza Januari 4 Uwanja wa Taifa
waligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2 na mchezo wa pili Yanga
ilishinda.
Morrison
amesema:”Unajua mimi sina utaalamu wa kupiga mipira iliyokufa hivyo niliamua
kupiga bila kufikiria nini kitatokea kwani ninamtambua mlinda mlango kazi yake
kuzuia hivyo sikudhani kama ningefunga.
“Bahati
nzuri niliukuta mpira nyavuni hilo lilinishangaza na kunifurahisha, furaha
ilikuwa kubwa kwa mashabiki na wachezaji hata tulipoingia ndani ya vyumba vya
kubadilishia nguo furaha ilikuwa kubwa,” alisema.
Morrison
akiwa amecheza mechi 10 za Ligi Kuu Bara sawa na dakika 900 amehusika kwenye
jumla ya mabao sita ya Yanga kati ya 31 akifunga mabao matatu na kutoa pasi
tatu za mabao.









HUNA JIPYA KIJANA NAONA UNAZID KUDHIHIRISHA UNAZI ULIOKUJAA KWENYE KICHWA CHAKO,POLE SANA ILA NIKUSHAURI KITU KAMA HUNA CHAKUANDIKA BASI ANDIKA KUHUSU KORONA,KAZI ZAKO ZOTE ZIMEPOTEZA MVUTO UNAANDIKA UWONGO MPAKA UNAPITILIZA,ETI MAKAMBO NI MALI YA YANGA,UNASTAHILI KUFUNGIWA BROTHER ILA SIJUI KUNA NANI HUKO JUU ANAEKUTETEA.
ReplyDeleteHuyu mwandishi sasa amejichoresha kabisa kichwani kwake kuna nini. Huyu anayemwita muusji wa simba kamtawala. Ukiwa mwandishi ficha mapenzi yako maana sasa unaonekana kama vile umeajiriwa na huyo morrison.
ReplyDeleteHujui labda kuna unyeti kati yake na huyo morison wake,hata ile aina ya ushangiliaji wake huyo morison inaleta mashaka,(mbinuko style)
ReplyDeleteMaropoko yale kwa yale kwa miezi Tele haki ya Mungu yanachefuwa Roho na imeshakuwa karaha Jitulizeni
ReplyDeleteHawa wanayo ile kujiona inferior mbele ya Mnyama wanahisi si kiasi chao kupata ushindi na wakipata shida inakuwa ndio kama hiyo
ReplyDeleteEnter your comment...
ReplyDeletestori za morisson kila siku!,tumezichoka
Mwaacheni limbukeni afurahie. Ni kama kuokota pochi. Lazima simulizi lirudiwe tena na tena.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteWanaoteseka wako wapi,kwa nini uteseke.Mikia inawauma mtulie dawa iwaingie Morison ni habari nyingine.
ReplyDelete