April 6, 2020



BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hakutarajia kumfunga mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula kwenye mchezo wa dabi iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Machi 8.

Kwenye mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 na mfungaji alikuwa ni Morrison alifunga bao hilo dakika ya 44 baada ya kuchezewa rafu na Jonas Mkude nje kidogo ya 18.

Ushindi huo uliifanya Yanga isepe na pointi nne mazima mbele ya Simba msimu huu wa 2019/20 na mabao matatu kwani kwenye mchezo wa kwanza Januari 4 Uwanja wa Taifa waligawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2 na mchezo wa pili Yanga ilishinda.

Morrison amesema:”Unajua mimi sina utaalamu wa kupiga mipira iliyokufa hivyo niliamua kupiga bila kufikiria nini kitatokea kwani ninamtambua mlinda mlango kazi yake kuzuia hivyo sikudhani kama ningefunga.

“Bahati nzuri niliukuta mpira nyavuni hilo lilinishangaza na kunifurahisha, furaha ilikuwa kubwa kwa mashabiki na wachezaji hata tulipoingia ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo furaha ilikuwa kubwa,” alisema.

Morrison akiwa amecheza mechi 10 za Ligi Kuu Bara sawa na dakika 900 amehusika kwenye jumla ya mabao sita ya Yanga kati ya 31 akifunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.

9 COMMENTS:

  1. HUNA JIPYA KIJANA NAONA UNAZID KUDHIHIRISHA UNAZI ULIOKUJAA KWENYE KICHWA CHAKO,POLE SANA ILA NIKUSHAURI KITU KAMA HUNA CHAKUANDIKA BASI ANDIKA KUHUSU KORONA,KAZI ZAKO ZOTE ZIMEPOTEZA MVUTO UNAANDIKA UWONGO MPAKA UNAPITILIZA,ETI MAKAMBO NI MALI YA YANGA,UNASTAHILI KUFUNGIWA BROTHER ILA SIJUI KUNA NANI HUKO JUU ANAEKUTETEA.

    ReplyDelete
  2. Huyu mwandishi sasa amejichoresha kabisa kichwani kwake kuna nini. Huyu anayemwita muusji wa simba kamtawala. Ukiwa mwandishi ficha mapenzi yako maana sasa unaonekana kama vile umeajiriwa na huyo morrison.

    ReplyDelete
  3. Hujui labda kuna unyeti kati yake na huyo morison wake,hata ile aina ya ushangiliaji wake huyo morison inaleta mashaka,(mbinuko style)

    ReplyDelete
  4. Maropoko yale kwa yale kwa miezi Tele haki ya Mungu yanachefuwa Roho na imeshakuwa karaha Jitulizeni

    ReplyDelete
  5. Hawa wanayo ile kujiona inferior mbele ya Mnyama wanahisi si kiasi chao kupata ushindi na wakipata shida inakuwa ndio kama hiyo

    ReplyDelete
  6. Enter your comment...
    stori za morisson kila siku!,tumezichoka

    ReplyDelete
  7. Mwaacheni limbukeni afurahie. Ni kama kuokota pochi. Lazima simulizi lirudiwe tena na tena.

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  9. Wanaoteseka wako wapi,kwa nini uteseke.Mikia inawauma mtulie dawa iwaingie Morison ni habari nyingine.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic