June 26, 2020


MIRAJ Atuman,’Sheva’ Kiungo mzawa mwenye uwezo mkubwa ndani ya Uwanja amesema kuwa bao lake alilowatungua Mbeya City anawaachia waamuzi kwa kuwa wao ndio wanajua kilichotokea.
Sheva Juni 24 Uwanja wa Sokoine wakati Simba ikishinda mabao 2-0 yote yakijazwa kimiana na nahodha John Bocco dakika ya 5 na 54, Sheva alifunga bao dakika ya 90+5 kwa pasi ya Clatous Chama,  lilifutwa na mwamuzi wa kati, Athuman Lazi kwa kile alichotafsiri kuwa mchezaji wa Mbeya City Keneth Kunambi alichezewa faulo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Sheva amesema kuwa hajui chochote kuhusu bao lake zaidi anamshukuru Mungu kwa kuwa timu yao imepata pointi tatu kibindoni.
“Goli langu mimi hata sijui inakuaje, hilo nawaachia waamuzi ila kikubwa ambacho ninafurahi kwa kuwa tumepata pointi tatu muhimu na maisha yanaendelea kwani kikubwa tunachohitaji ni pointi tatu hakuna kingine,” amesema Sheva.
Sheva kibindoni ana mabao sita na pasi moja ya mabao kati ya 69 ambayo yamefungwa na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 78 huku Mbeya City ikiwa nafasi ya 18 na pointi zake 30 zote zimecheza mechi 31.

5 COMMENTS:

  1. Lile lilikuwa ni hao halali, hakuna faulo yoyote sana sana mchezaji wa mbeya city ndio alifanya jaribio la kizuia mchezaji wa simba kwa njia isiyo sahihi na akadondoka mwenyewe

    ReplyDelete
  2. Kanjanja mmoja wa Mwanaspoti aliandika eti goli lilikataliwa kwa sababu Chama alimpiga mchezaji wa Mbeya City!!!Upenzi kwenye kuandika au udhaifu katika uandishi wa habari?Matatizo ya uandishi wa habari hasa za michezo ni mengi sana inatia aibu.Kuna mwandishi wa habari aliyemhoji mchezaji Morisson wa Yanga kwa kiingereza. Inatoa aibu level yake ya kuhoji kwa kiingereza. Angetafuta mkalimani.

    ReplyDelete
  3. Huyo kanjanja wa mwanaspoti hivi hakuona mabeki wa mbeya city walivyogongana mbona hajazungumzia goli la moringa alilofunga ameotea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hili la Moringa kwa kweli lina ukakasi mwingi Offside ya wazi lakini hakuna anayeongelea issue hii. Waandishi wa Bongo bwana!

      Delete
  4. AIBU KUBWA MAREFARII WETU MMEFELI. GOLI LA SHEVA GOLI HALALI KABISA. HAKUNA FAULO ILIYOFANYWA NA CHAMA. WACHEZAJI WA MBEYA CITY WENYEWE NDIO WAMEGONGANA MPIRA UKAENDELEA CHAMA AKACHUKUA MPIRA AKAUPIGA SHEVA AKAUPOKEA NA KUFUNGA BAO. REFA HUYU NA KIBENDERA WANAPASWA KUFUNGIWA KWA KUSHINDWA KUCHEZESHA KWA HAKI NA KULETA HALI AMBAYO INGEWEZA KULETA VURUGU UWANJANI. WAFUNGIWE MPAKA LIGI IISHE. WASUBIRI LIGI IJAYO.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic