June 26, 2020


BERNARD Morrison, nyota wa Klabu ya Yanga amesema kuwa alicheza mechi mbili akiwa hajasaini dili na klabu hiyo kwa kuwa walikuwa wakihitaji kutazama uwezo wake kwanza.

Morrison alitua ndani ya Yanga akiwa mchezaji huru akitokea nchini Ghana ambapo alisajiliwa kwenye usajili wa dirisha dogo la mwezi Januari.

Morrison amesema kuwa kazi alikubali kucheza mechi hizo kwa kuwa ana mapenzi na Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Luc Eymael.

"Nilicheza mechi mbili awali baada ya kuja Bongo ambapo ilikuwa ile ya kwanza mbele ya Singida United ambapo tulishinda baada ya hapo nikamalizana nao kwa kusaini dili na Yanga.

"Kuna mengi ambayo ninafanya na yote ni kwa mapenzi na klabu ya Yanga kwa kuwa huku tunashirikiana vizuri na tunaishi tukiwa ni familia ndio maana nikipata nafasi ninatimiza wajibu wangu bila matatizo," amesema.

Morrison ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa Uwanja wa Taifa kwa kuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi mbili kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons.

Akiwa amecheza mechi 11, Morrison ametupia jumla ya mabao matatu na ana pasi tatu za mabao ndani ya Yanga kwenye Ligi Kuu Bara.

7 COMMENTS:

  1. Kaka unajitahidi sana kuandika sasa tunaomba ufuatilie kwanini mchezaji acheze bila kuwa na mkataba alipataje kibali cha kufanyia kazi na ana mkataba na waajili wake.

    ReplyDelete
  2. Naomba mnisaidie, aliwezaje kucheza kabla hajasaliwa ai alisajiliwa kabla ya kusaini mkataba? Na kama timu alizocheza jazo yanga kwa kumtumia huyu zik8lalamika haitakuwa shida? Mwenye uelewa msuri anisaidie

    ReplyDelete
  3. ikiwa ni kweli morisoni alicheza hizo mechi pasipo kuwa na mkataba inabidi tff na yanga, watueleze ukweli maana hii ni ligi c ndondo cup maana inajulikana kibali cha kucheza lig kuu wanatowa tff sasa uyu aliwezaje kucheza pasipo kuwa na kibali au ilitumika ten pasent baina ya yanga na tff ? Ilo wanatakiwa tff na yanga walitolee ufafanuzi naikigundulika hakuwa na kibali cha kucheza lig kuu au yanga waliidanganya tff bac itolewe adhabu kali kwa yanga maana utakuwa ni uhuni ambao umepitiliza uyu morisoni kama yye ametamka hvyo tff na yanga waje watowe tamko hazarani hii ni aibu kwa taifa letu na lig yetu, leo morisoni akitoka hapa atatuona sisi watanzania ni 0 sasa wewe ulieandika makala hii ya morisoni tutawaona ni watu wazuri ikiwa mtawa tafuta tff watowe maelezo then na hawa yanga pia.

    ReplyDelete
  4. ni makosa ya TFF kuruhusu mchezaji acheze bila mkataba

    ReplyDelete
  5. Waandishi wanaandika wanachoambiwa badala ya kufatilia kama ni kweli pia kama ni kweli nani nani walihusika kuvunja sheria

    ReplyDelete
  6. Kama ni kweli ina masna Singida wana point za mezani toka Yanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Singida tawi kuu la Utopolo au umesahau issue ya Fei Toto ??

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic