June 4, 2020


DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa atapambana kuona timu yake inatwaa taji la Kombe la Shirikisho ili kuona timu yao inashiriki michuano ya kimataifa.

Nchimbi mbali na kucheza mpira yeye ni mkulima wa mpunga amesema kuwa kutokana na malengo ambayo wamejiwekea ana imani kuwa watafanya mambo mazuri kwa ajili ya furaha ya mashabiki na timu kiujumla.

Tayari Yanga imeanza mazoezi tangu Mei 27 ambapo wachezaji wote wapo kambini wakiendelea kujiweka sawa na mchezo wao wa kwanza wa ligi msimu huu baada ya miezi miwili kupita bila kucheza utakuwa dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Kambarage.

Sababu kubwa ya masuala ya michezo kusimama ni kuibuka kwa janga la Virusi vya Corona na kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza kwa kueleza kuwa maambukizi yamepungua.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nchimbi amesema kuwa anatambua kwamba mashabiki wanahitaji burudani jambo ambalo wamepanga kulifanya.

"Tupo vizuri na ligi inarejea hilo tunalijua, jambo kubwa ambalo tutapambana nalo kwanza ni kushinda mechi zetu za ligi na kushinda Kombe la Shirikisho ili kurejea kwenye michuano ya kimataifa," amesema.

Nchimbi ana mabao sita kibindoni akiwa amewatungua makipa watatu msimu wa 2019/20 na ana pasi mbili za mabao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic