AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa watakachokutana nacho leo Simba jioni saa 10:00 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara hawataamini kwani wamejipanga vizuri.
Said aliwahi kuitumia Simba enzi za uchezaji wake hivyo leo anakutana na mabosi wake wa zamani ambao anawatambua vema fasafa zake.
Mbeya City ina kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 4-0 mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, hivyo leo wataingia kulipa kisasi huku Simba ikipambana kusaka pointi tatu kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa.
Said amesema:"Wasitarajie kupata mteremko leo ndani ya uwanja, maandalizi yetu yapo tayari na kila mchezaji anajua majukumu yake hivyo kazi yetu ni moja kusaka pointi tatu."
3 point
ReplyDelete