June 24, 2020


TIMU ya Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hitimana Thiery mchezo wake uliopita wa Ligi Kuu Bara ikiwa Uwanja wa Majaliwa ilishinda mabao 2-0 mbele ya Kagera Sugar.

Leo itakutana na Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Luc Eymael ambayo ililazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC Uwanja wa Taifa.


Kwenye mchezo wao ambao walikutana Machi 15, mzunguko wa kwanza, Namungo ilitoshana nguvu na Yanga Uwanja wa Majaliwa kwa kufungana bao 1-1.


Bao la Yanga lilifungwa na Tariq Seif huku lile la Namungo FC likijazwa kimiani na Bigirimana Blaise na yote yalifungwa kwa vichwa.

Kinara wa utupiaji kwa Yanga ni David Molinga ana mabao nane huku Namungo, Relliants Lusajo akiwa na mabao 12.

Taifa wanakutana leo saa 1;00 Usiku huku vita kubwa ikiwa ni kwa upande wa nafasi na pointi tatu muhimu.


Yanga inahitaji kushinda ili kupunguza kasi ya Simba kutwaa ubingwa mapema na Namungo ikisaka nafasi ya kumaliza ndani ya nne bora.

Yanga kibindoni ina pointi 56 ikiwa nafasi ya tatu na Namungo FC ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 54 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic