July 18, 2020


INAELEZWA kuwa Manchester United wameamua kulifufua dili la kuisaka saini ya kinda anayekipiga Borussia Dortmund, Jadon Sancho huku wakihitaji kufanya makubaliano na mabosi wa wachezaji hao kwenye upande wa dau.
United walikuwa wanahitaji saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anayecheza nafasi ya winga kutokana na ubora wake alionao kwa sasa na Dortmund walikuwa wanahitaji euro milioni 100 jambo ambalo United liliwafanya wagome kuvunja benki.
Kocha Mkuu wa United, Ole Gunnar Solskjaer awali iliripotiwa kuwa anahitaji nyota huyo aungane na kiungo mshambuliaji Marcus Rashford pamoja na Mason Greenwood ili aongeze makali ndani ya kikosi hicho.
Ripoti zinaeleza kuwa United wanamtazama kwa ukaribu nyota huyo na wapo kwenye mkakati wa kufanya makubaliano na Dortumud ili kufanya makubaliano ya kuipata saini ya nyota huyo pale dirisha la usajili litakapofunguliwa Julai 27.
Sancho alijiunga na Dortmund mwaka 2017 akitokea Klabu ya Manchester City inaaminika kuwa anaweza kuondoka ndani ya timu hiyo msimu ujao. Hivi karibuni iliripotiwa kuwa hawana mpango wa kuisaka saini ya nyota huyo kutokana na dau kuwa kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic