BAADA ya
kupata ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Singida United, Uongozi wa Yanga umesema
kuwa umejipanga kuibuka na ushindi leo mbele ya Mwadui FC ili kuweka rekodi ya
kuichapa nje ndani.
Mchezo wa
kwanza walipokutana na Mwadui FC, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0
lililopachikwa na Balama Mapinduzi, leo wanakutana Uwanja wa Taifa kwenye
mchezo wa mzunguko wa pili.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa wamejipanga
vema kushinda mbele ya Mwadui FC ili wafikie malengo yao ya kumaliza ligi
wakiwa nafasi ya pili.
“Tupo tayari
kwa mchezo wetu dhidi ya Mwadui, bado tuna malengo ya kumaliza ligi tukiwa
nafasi ya pili hivyo ili tufikie malengo hayo ni lazima tushinde, mchezo wetu
uliopita dhidi yao tulishinda hivyo itapendeza tukiwafunga tena,” amesema.
Yanga ipo
nafasi ya pili ikiwa na pointi 67 inakutana na Mwadui FC inayopambana kujinasua
kushuka daraja ikiwa nafasi ya 17 na pointi 40 zote zikiwa zimecheza jumla ya
mechi 35.
Gongowazi hebu Kwanza vaeni fulana halafu ndio mjitambe na huku mmeshakosa kila kitu
ReplyDeleteAma kweli mumeyatimiza mmepiga njendani hongereni
ReplyDelete