August 18, 2020

 
HALI imeenda ndivyo sivyo katika usajili wa Eric Rutanga baada ya beki huyo kusema kuwa mabosi wa Yanga wamemchunia tangu asaini mkataba wa awali na timu hiyo.

 

Rutanga ambaye hapo awali alithibitisha kuwa amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ambapo alikuwa akisubiri kutumiwa tiketi ili kuweza kuwasili nchini.

 

Beki huyo amesema kuwa tayari alishasaini mkataba wa miaka miwili wa kukitumikia kikosi cha Yanga na baada ya hapo viongozi walimwambia atulie mipaka ikifunguliwa atatumiwa tiketi ya ndege jambo ambalo limekuwa tofauti mpaka sasa.


“Nilisaini mkataba na Yanga wa miaka miwili baada ya hapo viongozi wa Yanga waliniambia kuwa nisubiri mipaka ya Rwanda itakapofunguliwa lakini nashangaa hali imekuwa tofauti mpaka sasa.

 

“Nimekuwa nikiwatumia meseji lakini imekuwa kimya na hawajibu kabisa, hivyo nimekuwa na wasiwasi na dili hili ambalo nilikuwa nina uhakika nalo,” amesema beki huyo.

 

Dili la Rutanga na Yanga linaweza likaota mbawa kutokana na Yanga kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Polisi Tanzania, Yassin Mustapha.

8 COMMENTS:

  1. Acha kuassume taarifa zako uwe na uhakika unapoandika taarifa

    ReplyDelete
  2. we endelea kuchokonoa mambo yetu utaona.

    ReplyDelete
  3. Kama alishasaini wasiwasi wake ni nini? Je hakulipwa chake?

    ReplyDelete
  4. Walisema wa Msimbazi wahuni kwa kumchunia Shishimbi ambae yeye mwenyewe alitamka kuwa Hana haraka kwakuwa Ana ofa tatu lazima astadi vizuri kabla ya kuamuwa na huku Mnyama haraku Marinogo isipokuwa kazi ya chapchap Bila ya kubembeleza mtu

    ReplyDelete
  5. Kwan wachezaji wote wameshafika au usajili umeshafungwa? Kila kitu kinautaratibu wake, @Mwadishi anatafuta vierws kwa kutengeneza fitna...

    ReplyDelete
  6. Hiyo kishapotezewa ajiongeze. Ysnga wameona hana uwezo wa kupambana na wanaosajiliea upande wa pili. Kama alupewa kidhika uchumba zinatosha atafute dili jipya au ashitaki kea kupotezewa muda alipwe tena

    ReplyDelete
  7. Wanatambulishwa lini Makambo na Kotei, hawatajwi au ndio tena Ilikuwa propaganda zao eti kuwatia uchungu Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic