August 18, 2020


NAHODHA wa Klabu ya Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang amekubali kusaini dili jipya la miaka mitatu ndani ya Klabu hiyo.

Nyota huyo alikuwa kwenye mpango wa kuondoka ndani ya kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta ila kwa sasa ameonyesha nia ya kubaki kuendelea kukitumikia kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2020/21 na mshahara wake unatarajiwa kuwa pauni 250,000 kwa wiki.

Pia Arsenal inapiga hesabu za kupata saini ya beki wa Lille, Gabriel Maghalhaes ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho.

Arteta anahitaji kufanya mabadiliko makubwa ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa  Emirates ili kuwa na timu bora ndani ya Ligi Kuu England pamoja na michuano mingine. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic