August 12, 2020

 

BAKARI Mwamnyeto, beki mpya ndani ya kikosi cha Yanga, amesema kuwa atawashangaza wengi ndani ya kikosi hicho kwa kuwa wengi wanafikiri kwamba atashindwa kupata namba.

 

Mwamnyeto ni ingizo jipya ndani ya Yanga akisaini kandarasi ya miaka miwili kwa dau la milioni 220 ambapo inaelezwa kuwa milioni 70 aliziweka mfukoni mwake na milioni 150 zilikwenda Coastal Union.

 

Mwamnyeto alisema kuwa hana mashaka na suala la namba kwenye maisha mapya, anaamini uwezo wake na atawashangaza wengi.

 

“Wengi wana mashaka nami ila tayari nimeshafungua ukurasa mwingine wa maisha, nitapambana kuwa bora na wengi hawataamini watakachokiona, nipo tayari kwa ushindani.

 

“Nikiwa Coastal Union nimejifunza mengi pia nilicheza mechi nyingi ngumu na timu ilipata matokeo, hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka katika uwezo wangu,” alisema.

 

Kwa msimu wa 2019/20 Mwamnyeto alikuwa anawania tuzo mbili ambazo ni ile ya mchezaji bora na beki bora zote alikosa na kuibukia kwenye kikosi bora cha msimu wa 2019/20.

1 COMMENTS:

  1. Congratulations mwamnyeto, pambana ili kutimiza ndoto zako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic