UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa beki mpya aliyetambulishwa na Yanga Agosti 9 bado ana mkataba ndani ya timu hiyo yenye maskani yake Morogoro.
Kibwana amesaini dili la miaka miwili ndani ya Yanga ambayo ipo kwenye harakati za kuboresha kikosi kwa ajili ya msimu wa 2020/21 akibeba mikoba ya Juma Abdul ambaye hajaongezewa mkataba.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa Kibwana bado ni mali ya Mtibwa hivyo wanafuatilia ili wajue imekuaje mchezaji ametambulishwa Yanga.
Kifaru amesema:-"Shomari kijana mdogo ni mali ya Mtibwa Sugar bado ana mkataba ndani ya timu na inaonekana alidanganywa huko alikokwenda kwa kuwa haelewi hatma yake lakini sisi tunafuatilia kwa ukaribu.
"Siwezi kusema ana mkataba wa miaka mingapi ila ninachojua mimi ni mchezaji wa Mtibwa Sugar, ninawasiliana na mtu wa sheria ndani ya timu ili ajue mambo yatakuaje," amesema.
Hawa Utopolo wanasajili mchezaji mwenye mkataba tena bila uoga kwani wanajua wata play offer mentality ili waonekane wanaonewa. Mtibwa chukueni hatua huu mchezo lazima uishe.
ReplyDeleteWe Mkia hilo limeshatolewa ufafanuzi. Yanga imefuata utaratibu imeongea na viongozi waandamizi wa Mtibwa. Kama hao viongozi hawajamuarifu huyo mseamaji wao hayo ni mambo yao, hayaihusu Yanga. Mwaka huu mtapata tabu sana. Zusha jingine.
DeleteWee nyani kwani mwaka huu wa 2020 umeshaisha na unajisahaulisha na 4g?... endelea kusikilizia maumivu.
DeleteHi ni kiki ya mbwa was Simba aka mbwa was mooooo ambao mnataka jaja jaja za Morrison ili msishushwe daraja .....mpaka itaeleweka tu
ReplyDeleteMTIBWA SUGAR WALIKUA WAPI SIKU ZOTE HIZI ? HIZI NI NJAMA ZA SIMBA ILI YANGA IONEKANE INASAJILI WACHEZAJI WALIO NA MIKATABA NA CLUB ZAO !! WANADHANI WATANZANIA HAWANA AKILI AU HAWAJUI KUZICHAMBUA NJAMA ZAO!!! AZAM WALIISIFIA YANGA KUWA WAMEFANYA UUNGWANA KUWATAARIFU KUA WANAMTAKA SURE BOY NA LEO HAO HAO AZAM WANAILAUMU YANGA !!! MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA NA MWISHO WA SIKU MBIVU NA MBICHI ZITAJULIKANA TU
ReplyDeleteHuyo Tobias Kifaru anakurupuka. Yanga imefuata utaratibu imeongea na viongozi waandamizi wa Mtibwa. Kama hao viongozi hawajamuarifu huyo mseamaji wao hayo ni mambo yao, hayaihusu Yanga.
Deletewapuuuzi bhanaa
ReplyDeletekilaa upuuuzi waufanyao lazma waitaje Simba
sasaa hapo Simba kahusikajeeee
pumbaaaaaf zenyuuuuu
hv yanga mbona usajili wenu una shida hv kama hamna hela sii mtulie?
ReplyDeleteYanga anaharibu mambo kichaka cha lawama simba, inashangaza sana
ReplyDeleteKifaru hata muda wa mkataba wenyewe hajui eti atawasiliana na mtu wa sheria 😂😂 wenye kuendesha timu wameshachukua chao kama haujashirikishwa itakua bahati mbaya
ReplyDelete