August 12, 2020

 

KLABU  ya Tottenham inayonolewa na Kocha Mkuu, Jose Mourinho imekamilisha usajili wa kiungo Pierre-Emile Hojbjerg kutoka Southampton kwa dili la miaka mitano.

Kiungo huyo mwenye miaka 25 amejiunga na klabu hiyo kwa dau la thamani ya milioni 20 kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo amesanni dili la miaka mitano na amekabidhiwa jezi namba tano ambayo ataitumia msimu ujao wa 2020/21 kwenye Ligi Kuu England.

Nyota huyo alikamilisha utaratibu wa vipimo na kupewa dili hilo huku akionekana ni mwenye furaha ya kujiunga na kikosi hicho na amesema kuwa anafurahi kuwa ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo amesema:"Kwangu naona ni njema hasa kusaini mkataba wa miaka mitano na kupewa jezi namba tano nadhani ni jambo la kufikirika na litakuwa na upana wa matokeo mazuri hapo baadaye.


: "Ninajifunza vingi na ninaamini nitaendelea kujifunza mengi ndani ya timu yangu mpya kikubwa ni ushirikiano na kufanya kazi kwa juhudi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic