August 12, 2020

 

KIUNGO wa Yanga Bernard Morrison ametuma ujumbe kwa mashabiki wake akiwataka washushe presha kwa sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Morrison ametupia video akionekana akichezeza mpira na kuweka ujumbe uliosema kuwa:" Tulieni msiwe na presha,"

Kwa sasa Morrison yupo kwenye mvutano mkubwa na Yanga kuhusu suala lake la mkataba ambapo shauri hilo limeanza kusikilizwa Agosti 10 na 11. Siku zote mbili hakuna majibu ambayo yalitolewa zaidi ya maelezo kuwa bado shauri linaskilizwa.

Leo Agosti 12 linatarajiwa kuskilizwa tena na hukumu inatarajiwa kutolewa leo na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).

Shauri hilo pia lina mvutano mkubwa baada ya Simba kumtangaza mchezaji huyo Agosti 8 kuwa mali yao ilihali alikuwa ana kesi haijatolewa hukumu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic