August 15, 2020

 


SIXTUS Sabilo, mshambuliaji aliyekuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania ametambulishwa leo Agosti 15 ndani ya Namungo FC kwa dili la mwaka mmoja.


Sabilo alikuwa kwenye hesabu za kuibukia Yanga ambao walimuahidi kumfuata baada ya ligi kuisha ila ligi ilipoisha mambo yakabadilika.


Mkataba wake wa mwaka mmoja ndani ya Polisi Tanzania inayonolewa na Malale Hamsini umekwisha hivyo amejiunga Namungo akiwa mchezaji huru.

Amesaini dili la mwaka mmoja kwa kikosi cha Namungo chenye maskani yake Lindi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic