Larry Bwalya mwenye miaka 25 yeye ni kiungo mshambuliaji anakipigandani ya Ligi Kuu ya Zambia kwenye Klabu ya Power Dynamos anahusishwa kujiunga na Yanga na inaelezwa mazungumzo baina ya pande zote mbili yanaendelea vizuri.
Walter Bwalya mwenye miaka 25 huyu ni mshambuliaji wa zamani wa Nkana FC (The Red Devils) kwa sasa anakipiga Ligi Kuu ya Misri kwenye Klabu ya El Gouna FC yeye anahusishwa kujiunga na Simba.
Kwa muda mrefu Bwalya amekuwa akitajwa kuibukia Simba ila kikazwo awali ilikuwa inatajwa kuwa ilikuwa ni dau kubwa ila kwa sasa mambo yanaelezwa kuwa safi kwa pande zote mbili kuelewana.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wapo vizuri katika masuala ya usajili wana imani ya kuwa na kikosi bora cha ushindani.
Unatuzuga unawaelekeza Simba kuhusu Larry Bwalya ambaye yupo na Yanga ????? Bwalya mwingine hamumuwezi kwa za MO ENERGy
ReplyDeleteLARRY BWALYA yupo dar kwa ajili ya mazungumzo ya kujiunga na Simba. Mwandishi wewe ni mmoja wa maadui wakubwa wa Yanga, umekuwa ukitumika kuwasajilia Simba kupitia mgongo wa Yanga, lengo lenu ni kuidhoofisha Yanga kwakuwa mna amini Simba imara itaonekana mbele ya Yanga iliyo dhaifu. Wewe ni mtu hasidi sana kwa Yanga sema hawajakushtukia tu.
ReplyDeleteLarry Bwalya ameshamalizana na Simba, amesaini mkataba wa miaka miwili. Simba wamefanya kweli wakati Yanga walikuwa wanadanganya tu kuwa wanafuatilia.
ReplyDelete