August 15, 2020

 

 DAVID Kameta maarufu kama Duchu leo Agosti 15 ametambulishwa rasmi ndani ya kikosi cha Simba.

Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Bara akitokea Klabu ya Lipuli.

Kwa msimu wa 2019/20 akiwa Lipuli ambayo itashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao alitupia mabao matatu na kutoa jumla ya pasi saba.

Anaungana na Shomari Kapombe ambaye ni beki wa kulia ambaye naye ni mtambo wa kumwaga maji.

Msimu wa 2019/20 ametoa jumla ya pasi sita kati ya mabao 78 yaliyofungwa na Simba.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic