August 16, 2020

 

DAVID Molinga, mshambuliaji namba moja ndani ya Klabu ya Yanga kwa msimu wa 2019/20 amesema kuwa hakupenda kuondoka ndani ya kikosi hicho mapema.


Akiwa ndani ya Yanga, Molinga alitupia jumla ya mabao 11 na kutoa pasi moja ya bao kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar wakati Yanga ikishinda bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba.


Tayari kwa sasa ameshakwea pipa kurejea Congo baada ya Ligi Kuu Bara kuisha na mabosi zake Yanga kumpa mkono wa kwa heri baada ya mkataba wake kuisha hawajamuongezea dili jingine.


Nyota huyo amesema kuwa alipewa matumaini ya kubaki msimu ujao ila hakushtuka alipoambiwa kwamba ameachwa kwa kuwa ni sehemu ya maisha ndani ya soka.


"Bado nilikuwa ninapenda kubaki ndani ya Yanga ili niendelee kuonyesha uwezo wangu ambao ninao ila kwa kuwa sikuwa na chaguo baada ya kuachwa basi nitakwenda kuangalia changamoto nyingine.


"Ninachojua mimi bado nilikuwa nina nafasi ya kufanya makubwa zaidi kwa msimu ujao ukizingatia kwamba ni msimu wangu wa kwanza na uwezo wangu umeonekana,hamna namna ninaondoka nina amini nitapata timu sehemu nyingine," amesema.

2 COMMENTS:

  1. Pole kaka hao ndio kandambili aka vyura aka GONGOWAZI pole sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kelele zote za Nini? MIKIA FC bana! Mbona mliokuwa mnatembeza BARAKOA so tukawakaushia.WW Kilaza kweli kweli.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic