August 16, 2020

 


SHARAF Shiboub,  kiungo wa Simba aliyeibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Sudan, shujaa wa mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Azam FC anatajwa kuingia anga za Yanga ambao wanazidi kuimarisha kikosi chao.


Habari zinaeleza kuwa Yanga wanatambua kwamba kiungo huyo hayupo kwenye hesabu za Simba msimu wa 2020/21 hivyo itakuwa rahisi kumpata wao akiwa mchezaji huru.

Mkataba wake wa mwaka mmoja aliosaini ndani ya Simba tayari umekwisha meguka na hajaongezewa mkataba mwingine mpaka anaibukia kwao nchini Sudan.

"Kabla hajaondoka Bongo kuna watu wa Yanga ambao walimfuata Shiboub na kuzungumza naye, waliweka dau mezani ila nyota huyo hakuwaelewa zaidi ya kuwaambia waongeze dau hivyo wanasubiri Simba waachane naye kabisa maana wakisema wawafuate kwa sasa watatajiwa bei ya kukomoa," ilieleza taarifa hiyo. 


Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa Shiboub hana nafasi tena ndani ya kikosi hicho licha ya uwezo wake kuwa mkubwa alionyesha jeuri baada ya kurudi wakati ule janga la Virusi vya Corona lilipotulia.


"Shiboub ni mchezaji mzuri lakini ishu ya kuongezewa mkataba Simba itakuwa ngumu, ile likizo ya Corona ilimuongezea kiburi aliporudi alibadilika kidogo tofauti na mwanzo sasa maisha ya jeuri ndani ya Simba hayana nafasi ndio maana unaona hakucheza hata mechi moja, safari inamhusu," ilieleza taarifahiyo.


Ndani ya Ligi Kuu Bara,  Shiboub ametupia mabao mawili na kutoa jumla ya pasi sita za mabao kati ya 78 yaliyofungwa na timu yake ya Simba.

8 COMMENTS:

  1. Mabingwa wa G4 wanao wazuri kuliko huyo sana na hakupata nafasinna na ndio mana akatemwa. Ganda la muwa la Jana, chungu kaona uhondo

    ReplyDelete
  2. kitendo cha mchezaji kupewa haki angali na mkataba halali kutasababisha kuwashawishi wachezaji wengine wavunje mikataba hovyo wakitegemea kinga ya viongozi wenye nguvu za kisiasa na za pesa aina ya (Hanspope na Mo) na huku ndio kuharibu soka letu maana hata hizo 4G wanazotamba simba hazikutokana na uwezo wao bali ni kwa kuwarubuni wachezaju wa Yanga ndio sababu wakicheza na tim kkubwa wanapigwa KHAMSA na hata suala la morisson lilishasemwa na Manara kabla ya miezi chungu nzima na wapenzi wa soka hawajasahau wanajua kilichokua kikifanyika. nawapongeza Yanga kwa kugundua hilo na kuwatoa wachezaji Mamluki na wanaosababisha migomo ya mara kwa mara - povu rukha ili tufundishane na kujua ukweli

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mlifungwa 6-0 na simba mkasema mlibadilisha kikosi kizima ndiyo sababu ya kufungwa goli hizo , mkafungwa 5-0 na simba, marehemu mzee Akilimali akasema kuwa eti kwa kuwa wazee walivua kofia ndo mana mkafungwa goli hizo, leo tena mmefungwa 4-1(hii ni mara ya tatu mara ya tatu)mnasingizia Simba inawarubuni wachezaji wenu , eti simba akicheza na timu kubwa anapigwa hamsa mbona husemi baada ya kupigwa hizo hamsa aliyepita kucheza robo fainali ni nani mbona huzungumzii kipigo tulichompa Js Soura 3-0 na wao tuliwarubuni wachezaji wao? mbona Al Ahly ailpigwa 6-0 na Mmamelodi Sundowns naye huwea narubuni wachezaji kwenye ligi ya nitajie we mwaka gani Yanga kashawahi kuifunga timu ya kiarabu zaidi ya goli mbili , eti ili tufundishane na tujue ukweli, mzoea vya kunyonga kuchinja haviwezi mlishazoea kubebwa kipindi cha Malinzi ndiyo mana maneno yote yanawatoka kipindi cha Malinzi ndiyo yalitokea mambo mengi ya ajabu kwenye mpira wetu tuliona Ndanda alivyocheza mechi mbili za ligi kwenye uwanja wa Taifa, tuliona Rais wa TFF (Malinzi) aki tweet Yanga wanaongoza ligi, mmesahau ya Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Ramadhan Kessy leo hii nyinyi mmekuwa wasafi sana ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni!!!

      Delete
    2. kuna yamkini aliyosema Eymael kuhusu nyani.,ligi za mabingwa 2019...walipata nafasi kupitia mgongo wa Simba...
      Simba ilipoteleza ikawa ni vicheko...kana kwamba Simba ilitolewa kwa kufungwa na UD Songo...
      Wao wakaja kutolewa kwa kujifunga wenyewe Zambia!

      Delete
  3. Huyo hakuwa wa halali kwasababu saini ya hiyo ya miaka miwili haikuwa yake na baadae ikafutwa na huyo aliyeitia ajiweke tayari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic