August 21, 2020


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa anawapenda mashabiki wa Yanga kwa kuwa ni wavumilivu ila kitendo cha kumbeba kiongozi wao juu ni tukio la hovyo,


Jana Agosti 20, Yanga waliwapokea wachezaji wake wapya wawili ambao ni Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko wote kutoka AS Vita na kwenye mapokezi hayo Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Mwekezaji kutoka Kampuni ya GSM alibebwa juu mithili ya mfalme.

Manara ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na kituo cha +255 Global Radio ambapo amesema kuwa anaamini mashabiki wa Yanga ni wavumilivu. 

 " Kitu pekee ambacho nakipenda Yanga ni kuwa wana moyo wa chuma, ni wavumilivu hasa, kwa matokeo yale wanayopata huku wanambeba kiongozi wao juu, ni tukio la hovyo kabisa lile.” 


16 COMMENTS:

  1. wanaleta tabia za kitumwa karne hii kweli utopolo fc yule kocha kuwaita Yale majina flani hvi alijuwa tabia zenu zina endana 😂😂😂

    ReplyDelete
  2. Manara wewe mnafiki Na mzandiki hata kwenye dini pia walisemwa watu kama wewe.sasa wewe ulipomfunga viatu Morisson ni tukio sahihi like,

    ReplyDelete
  3. Kumsaidia mtu kufunga kamba sio sawa na tukio tulilolifanya sisi. Imeleta picha za enzi za utumwa.Mimi ni Yanga lakini tukio hilo sio sawa.

    ReplyDelete
  4. Hivi Mwl.Nyerere alipobebwa juu kwa juu na wakazi wa Dar es Salaam wakati aliporudi toka UN ilikuwa ni kuendekeza enzi za utumwa?

    ReplyDelete
  5. Utumwa ni kutumikishwa kazi bila ridhaa yako je wale waliombeba Hersi walilazimishwa? Ni wivu tu

    ReplyDelete
  6. Nadhani kadri siku zinavyoenda mdogo wangu Haji anatindikiwa uwezo wa kutunza kumbukumbu je yeye mwenyewe alipobebwa na mashabiki wa Simba walikuwa watumwa wake?
    Au siku ile wamembeba kocha wao wa kizungu ilimaanisha yeye ni mfalme na wao Simba watumwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwasababu amechukuwa kombe nyie mmembeba kwa ajiri gani?

      Delete
  7. Utumwa ni kumfanyisha mtu kazi bila ridhaa yake. Je waliombeba Hersi walilazimishwa? Ni wivu tu

    ReplyDelete
  8. Kimsingi hapakuhusu wewe hangaika na yako kuifuatilia yanga ni kupoteza muda kwa kuwa ina wenyewe. Unayoyafanya wewe ni mengi ya hovyo hatukusemi kwa kuwa ni maamuzi yako, kama yanga walivyombeba SAIDI.

    ReplyDelete
  9. Lakini ipi ya karaha zaidi. Unaweza kumbeba Mzee wako ikihitajika au mtoto wako mdogo ni lazima au mgonjwa ni jambo la thawabu na wajibu lakini kulibeba baba sawa na wewe kwa kila kitu kwa kweli karaha hata kutazama

    ReplyDelete
  10. Hivi tunakwama wapi Tz, enzi hizo watu mashuhuri walibebwa kwa sababu hakukuwa na usafiri kama wakati tulio nao sasa. Leo hii kulingansha kubebwa kwa Nyerere aliyetuletea uhuru na mtu aliyeleta wachezaji ambao hata uhakika wa ku-perform hatuna ni kuonyesha jinsi akili zilivyo ndogo. Tungejiongeza kidogo tu tukatumia umati kama huo kuugeuza kuwa uchumi wala tusingebabaika na magarasa kama hayo. Badala ya kupoteza muda uwanjani tujaribu kuchangia timu walau elfu moja tu tutaweza sajili wachezaji wazuri wengi tu na tutaachana na ushamba wa kubeba wasanii kwa kuleta wachezaji ambao timu yao imeona hawatakuwa na msaada kwenye kusaka ubingwa wa Afrika badala yake waje wagombee Mapinduzi cup!

    ReplyDelete
  11. Msemeni huyo Haji ila mi nauliza kwani amewapa nini kila kitu anajua yeye,alafu ninyi akina Salehe hata press conference ni kama mnampangia hongea hivyo msitufanye tumtukane Hana haki ya kutupangia Cha kufanya na yet siyo regulator we respect him bt this is too much Kama alisingiziwa babake Kuna siku tutampa adabu

    ReplyDelete
  12. Hata ile staili iliyotumika kumbeba ndio inaleta ukakasi zaidi. Bora wangembeba tuu kwa mabega na mikono lakini sio kumwandalia kiti kivile imaleta taswila ya kitumwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic