August 21, 2020


MWENYEKITI wa Bodi ya Klabu ya Simba na Mwekezaji Mohammed Dewji amesema ameagiza vifaa kwa ajili ya kuwamonitor wachezaji wake (GPS). 

Mo amesema hayo leo, Agosti 21 kwenye mkutano na Waandishi wa Habari akisema kuwa malengo ya kufanya hivyo ni kujua mienendo ya wachezaji ndani na nje ya uwanja.

Ameongeza kuwa malengo ya Simba kwa msimu huu ni kuweza kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Malengo yetu sasa ni kuendelea kushindana ndani na kushinda ubingwa lakini pia kufika kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mipango yetu mwaka huu ni kujenga hosteli za timu, uwekezaji wa GPS ambao tutakuwa tunaona takwimu za wachezaji.

" Vifaa hivyo vitaweza kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa mchezaji, amelala saa ngapi, mapigo yake ya moyo, kama akitumia kilevi na sehemu aliyopo pamoja na vitu vingine vingi," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Mhhhhh!!!!!!Hivi vifaa imekuwa ni vya kufungwa wachezaji tena!! Nimewaza wale faru waliofungwa GPS na magari ya makampuni yaliyofungwa hivyo vifaa ili kufuatilia mienendo yao nimebaki najiuliza kama kuna tija katika huo mpango.

    ReplyDelete
  2. mbona kama inaingilia haki ya faragha ya mtu....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Well said ndugu....Huko ni kuingilia faragha za watu,ikumbukwe wachezaji ni binadamu wenye akili timamu na wanatambua majukumu yao sidhani kama ni muafaka kuwafunga ving'amuzi ili kujua mienendo yao,suala la muhimu ni kuwaambia ukweli ili wajitambue na kama ikitokea baadhi yao hawajali taratibu zilizowekwa na timu basi hakutakuwa na sababu ya kuwa nao

      Delete
  3. Tatizo hamjui kilichozungumzwa. Na ndio tabu ya ku assume. Mashine hizi zinapima mchezaji amefanta mazoezi kwa muda gani na kwa ufanisi kiasi gani?
    Wachezaji wavivu na wasiowajibika kwenye mazoezi wataumbuka kwa level zako zitaonekana wazi wazi.
    Haina maana watafungwa GPS bali kinatumiwa wakati mazoezi kupims fitness level yako baada ya kupewa majukumu.
    Wachezaji wanalipwa ni lazima walinde miiko ya kazi zao na miili yao wanapokuwa kazini.
    Chukulia mfano wewe ni dereva wa basi la abiria unakwenda kazini umelewa unafikiri mwenye basi atakuambia hiyo ni private life yako,?
    Wachezaji wakati wakuwa kazini wafuate miiko ya mpira ambao ndio kazi yako sio burudani.

    ReplyDelete
  4. We ushaambiwa hao ni manyani fc hata uwaambie kitu gani hawaelewi hiyo technology wanatumia wenzetu waliondelea hao watabaki kuwa ni manyani fc for ever

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic