August 1, 2020


SHIZA Kichuya maarufu kama chakaramu kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Simba inaelezwa kuwa  msimu ujao atakipiga Namungo FC kwa mkopo baada ya kushindwa kufurukuta ndani ya kikosi hicho.

Kichuya chini ya Sven Vandenbroeck hajawa na msimu mzuri baada ya kujiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Klabu ya ENPPI ya Misri.

Amecheza jumla ya mechi tano ambazo ni sawa na dakika 450 huku akifunga bao moja mbele ya Ruvu Shooting kwenye sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Taifa.

Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa hakuna nafasi kwa kiungo huyo kukipiga ndani ya Simba msimu wa 2020/21 hivyo anaweza kutolewa kwa mkopo ama akaachwa mazima.

"Nafasi ya Kichuya imeisha ndani ya Simba kwa msimu ujao, hajawa yule ambaye walimtarajia hivyo benchi la ufundi ndilo litaamua hatma yake lakini kwa namna mambo yanavyokenda ndo imeisha hiyo.

"Anaweza kupelekwa Namungo huko akacheze maana ndio sehemu ambayo wachezaji wengi wa Simba wanapelekwa lakini kusema kwamba atabaki hilo hata halina nafasi," ilieleza taarifa hiyo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia masuala ya wachezaji watakaochwa kwa kuwa wakati wake bado haujafika.

“Siwezi kuzungumza kwa sasa kuhusu wachezaji ambao wataondoka ndani ya Simba, bado wakati haujafika mambo yakiwa sawa kila kitu kitawekwa wazi,” amesema.

1 COMMENTS:

  1. Tetesi kila siku - Kichuya kwa mkopo Namungo; Rashid Juma kwa mkopo Polisi. Tutasikia mengi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic