August 12, 2020

 

Azam FC leo Agosti 12 imeingia mkataba wa miaka miwili na beki wa kushoto, Emmanuel Charles, akitokea Mbao kwa usajili huru.


Charles usajili wake ni sehemu ya kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi la Azam FC, likiwa ni pendekezo la benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioaba.


Beki huyo alikuwa na kiwango bora akiwa na Mbao msimu uliopita, akifanikiwa kutengeneza mabao matatu na kufunga mawili.


Huo ni usajili wa sita kwenye kikosi cha Azam FC kuelekea msimu ujao, wengine wakiwa ni kipa David Kissu, Awesu Awesu, Ally Niyonzima, Ismail Aziz na Ayoub Lyanga.


Zoezi la usajili litafungwa na kikosi hicho kwa kumalizia nafasi mbili za wachezaji wa kigeni, wanaotarajiwa kutua nchini hivi karibuni.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo makubwa ni kuboresha timu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic