NYOTA wa zamani wa timu ya Taifa ya England na Manchester United, Rio Ferdinand amesema kuwa kwa kichapo cha mabao 8-2 walichokipata Barcelona kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Bayern Munich usiku wa kuamkia leo ni tiketi ya Lionel Messi kuondoka.
Licha ya jitihada za mshindi wa Ballon d'Or, Messi kusaka ushindi hazikuzuia kichapo hicho cha udhalilishaji kwenye mchezo huo na kuwafanya waishie hatua ya robo fainali ya mashindano hayo makubwa duniani.
Ferdinand ambaye pia ni mchambuzi wa BT Sport amesema kuwa anaamini kuwa Messi anaweza kuondoka Nou Camp kwa kuwa amekuwa akipishana na mataji mengi jambo ambalo linamfanya asiwe na furaha ndani ya kikosi hicho.
Mvua ya mabao ya Bayern Munich ambao ni mabingwa wa Bundesliga ilianza dakika ya nne kupitia kwa Thomas Muller aliyefunga mabao mawili na lingine alifunga dakika ya 31,Ivan Perisic dakika ya 21,Serge Gnabry dakika ya 27,Joshua Kimmich dakika ya 82,Phillippe Coutinho naye alitupia mawili dakika ya 85 na 89.
Yale ya Barcelona yalifungwa na David Araba ambaye alijifunga dakika ya 7 na Luis Suarez mshambuliaji wa Barcelona dakika ya 57 na kuwafanya watoke uwanjani kinyonge kwa kuchapwa mabao mengi ambayo yamewaumiza.
"Kwa sasa Messi atakuwa na maswali mengi kichwani, nadhani atafikiria kuondoka kutokana na mwendo ulivyo, yupo kwenye wakati mgumu hasa pale anapotazama uwezo wake na uwezo wa kikosi nadhani atafikiria kuondoka," amesema Rio.
0 COMMENTS:
Post a Comment