LEO hii majira ya saa 1:30 usiku pazia litafungwa kwenye moja ya mashindano maarufu Uingereza na Ulaya,kwa kushuhudia mchezo mkali kati ya Arsenal na Chelsea.
Fainali ya kombe la FA itafanyika katika uwanja wa Wembley wakati mahasimu wawili Arsenal na Chelsea watakuwa wakiwania taji la mwisho kwa msimu huu.
Klabu zote zimezitoa timu mbili imara kwenye hatua ya nusu fainali za kombe la FA –United na City.
Timu ya Mikel Arteta iliwaondosha Manchester City kwa goli 2-0 katika hatua ya nusu fainali, wakati kwa upande wa Chelsea iliwatoa Manchester United kwa 3-1 katika hatua hiyo hiyo ya nusu faianali.
“The Gurners” mara ya mwisho kufika fainali za kombe la FA ilikuwa mwaka 2017 na kupata ushindi dhidi ya Chelsea, wakati Chelsea ikiwa ni timu iliyoshinda mara nane FA Cup ilifanikiwa kufika fainali kwa mara ya mwisho mwaka 2018.
0 COMMENTS:
Post a Comment