Inter Milan ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 5-0 mbele ya Shakhtar Donetsk kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali.
Nyota ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Lukaku imekuwa kali kwani alifunga mabao mawili sawa na Martinez huku moja likifungwa na D'Ambrosio.
Inakutana na Sevilla ambayo ilishinda mabao 2-1 mbele ya Manchester United ambao bado hawataki kuamini kama walinyooshwa mabao hayo na wapinzani wao.
Kwa Inter Milan inakuwa ni mara ya 10 kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Europa huku kibarua cha Kocha Mkuu, Antonio Conte kikiwa kimeshikiliwa kwa muda kwa kuwa inaelezwa kuwa anaweza kutimuliwa ikiwa hatashinda taji lolote msimu huu.
Fainali itapigwa Uwanja wa RheinEnergieStadion nchini Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment