TUISILA Kisinda na Tonombe Mukoko wachezaji wapya wa Klabu ya Yanga wanatarajiwa kuwasili nchini leo Agosti 20 majira ya saa saba mchana.
Nyota hao wote ni washkaji walikuwa wanakipiga pamoja ndani ya Klabu ya AS Vita ya Congo hivyo wanakuja Bongo kuendeleza ushkaji wao pamoja na kazi.
Wote wawili wamesaini kandarasi ya miaka miwili na mabosi wa Yanga kwa kushirikiana na Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa timu hiyo walikuwa wakisimamia kila kitu kiende sawa.
Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM amesema kuwa usajili wa nyota hao ni mzuri na wataendelea kufanya usajili kwa kuwa muda upo.
"Tumefanya usajili mzuri kwa kumalizana na viungo wazuri ila bado tunahitaji mshambuliaji mmoja ambaye atakuwa anasimama katikati, hivyo kabla ya wiki ya Wananchi tutakuwa tumefanya jambo letu," amesema.
Nyota huyo ambaye anatajwa kuingia anga za Yanga ni Carlos St'enio Fernandez raia wa Angola ambaye ni mshambuliaji.
Dirisha la usajili lilifunguliwa Agosti Mosi na linatarajiwa kufungwa Agosti 31.
0 COMMENTS:
Post a Comment