HAWA ni marafiki wa kitambo sasa wanaendelea kuwa marafiki ndani ya timu zao mpya namna hii:-
Awesu Awesu v David Kissu
Wote wapo zao Azam FC. Walikipiga pamoja Singida United msimu wa 2008/19, Kisu msimu uliopita alikuwa Gor Mahia na Awesu alikuwa Kagera Sugar sasa wote wapo Azam FC.
Joash Onyango v Francis Kahata
Wote ni raia wa Kenya, Kahata na Onyango ni washakji kutoka ndani ya timu ya Taifa ya Kenya, 'Harambee Stars' alianza kuibuka Kahata msimu wa 2019/20 kisha Onyango kamfuata mshikaji wake ndani ya Simba 2020/21.
Kapama, Materema na Ufudu
Nyota hawa walikuwa washkaji ndani ya JKT Tanzania msimu wa 2018/19, msimu wa 2019/20 wakatengana Materema alibaki JKT Tanzania, Ally Nassor,'Ufudu' aliibukia Mbeya City na Nassor Kapama akaibukia Kagera Sugar ila sasa wote wapo Kagera Sugar
Bwalya v Chama
Ni washakji kutoka timu ya Taifa ya Zambia,' Chipolopolo' sasa wote wawili, Larry Bwalya na Clatous Chama wanaendeleza urafiki ndani ya Simba msimu wa 2020/21.
Kalambo na Peter Mapunda
Aron Kalambo na Mapunda walikuwa washkaji ndani ya Mbeya City na sasa wapo pamoja ndani ya Dodoma Jiji.
0 COMMENTS:
Post a Comment