August 12, 2020

 ULINZI mkubwa ulitawala jana kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison akisubiria hukumu yake.

Hiyo ikiwa ni siku ya pili tangu kiungo huyo afikishwe kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kutokana na matatizo yaliyoonekana kwenye mkataba wake na Yanga.


Kamati hiyo ilikutana juzi asubuhi na kufanya kikao kizito ambacho kilianza juzi Jumatatu asubuhi na kumalizika usiku, lakini hakikutoa majibu na jana walikutana tena kuanzia asubuhi.

 

Hata hivyo, kulikuwa na ulinzi mkali sana baada ya difenda mbili zikiwa zimejaa askari kuingia eneo hilo ambapo moja ilidumu kwa muda mchache na kuondoka.

 

Awali ilielezwa kuwa Morrison alisaini mkataba wa miezi sita na timu hiyo, lakini wakati inaelezwa kuwa anaweza kujiunga na Simba, Yanga walisema kuwa wamempa mkataba wa miaka miwili.

 


Hata hivyo, kabla ya kumalizika kwa sakata hilo, Simba waliweka picha ya kiungo huyo kwenye mtandao wao akiwa anasaini.

 

Hakuna mtu yeyote ukiachana na viongozi wa kamati hiyo au wale wa TFF ambao walikuwa wanaruhusiwa kusogea karibu na geti la ofisi hizo jana, sehemu ambayo ilikuwa na walinzi ambao siku zote wanalinda kwenye geti hilo

 

Kiungo huyo jana alifika kwenye shirikisho hilo saa saba mchana na moja kwa moja kuingia katika ofisi hizo, tayari kwa ajili ya kuendelea na kesi hiyo ambayo ilikaa hadi saa 10: 10 jioni.Baada ya hapo askari walitoka na kuwaondoa mashabiki wote waliokuwa wamejazana nje ya geti hilo.


Leo Agosti 12 maamuzi ya ishu ya sakati hilo yanaarajiwa kutolewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic