August 12, 2020

 

MWENYEKITI wa zamani wa Simba ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) Ismael Rage amesema kuwa sakata la Bernard Morrison ni jepesi ila mambo yanakuzwa kuwa makubwa.

Rage amesema:"Yanga wangeweka mkataba hadharani kama wanao. Kwangu Yanga wamepigwa bao la kisigino. Maana kuna ushahidi alicheza mechi mbili kabla ya kuwa na kibali.

"Ndio maana nimesema hili suala ni jepesi sana na ninawatahadharisha TFF, maana kuna TMS Manager ambaye anacontrol namba. Anayeingia anakuwa ana namba yako, kama ukitaka kuingia yaani yule meneja, maana yake TFF nao wanaona. 

"Sasa isije ikawa mchezo huu umechezwa na TFF wameona maana yake itakuwa fedheha kwa nchi na TFF yenyewe, " amesema  Rage. 

Leo kesi ya Morrison inatarajiwa kutolewa hukumu baada ya kuskilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Ilianza Agosti 10 kuskilizwa makao makuu ya TFF pale Karume ikaendelea Agosti 11 na leo Agosti 12 inaendelea kuskilizwa na majibu yanatarajiwa kutolewa leo.

1 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo mwenye makosa ni TFF na sio Yanga maana TFF ndio wenye funguo ya kumfungulia mchezaji aingie ndani au atoke nje baada ya kuingia.Swali la pili kama Morrison alikuwa anacheza ina maana alipata leseni ya mchezaji toka TFF je ni nani alitoa hiyo leseni?na kama hakuwa na leseni aliruhusiwa vipi kucheza mechi?kwenye ukaguzi wa leseni kabla ya mechi alikuwa anaonesha nini? Kwa mtazamo wangu tatizo lipo TFF wala si kwa vilabu na inabidi wawajibishwe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic