August 12, 2020

 SERIKALI imesema kuwa inashangaa na suala la maamuzi ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison kucheleweshwa kutolewa hukumu.


Mwakyembe amesema kuwa suala hilo likifika mikononi mwaka atatumia dakika 10 kutoa maamuzi.

Sakata la Morrison limeanza kuskilizwa Agosti 10 na 11 ambapo hakukuwa na majibu kutoka kwa Kamati ya Hadhi za Wachezaji kuhusu mvutano wa kimkataba kati ya mchezaji huyo na timu yake ya Yanga.

Leo Agosti 12 pia linaendelea kuskilizwa kukiwa hakuna majibu yoyote licha ya jana kamati kuahidi kutoa majibu majira ya saa saba.

Waziri wa Michezo, Harrison Mwakyembe amesema kuwa anashangazwa na kuona namna mambo yanavyokuwa magumu kwenye maamuzi jambo ambalo linapoteza muda mwingi.

"Suala la mkataba lipo wazi inanishangaza kuona mpaka sasa hakuna maamuzi ambayo yametolewa mpaka sasa ndio maana inapelekea kuwe na taarifa kwamba ndani ya timu kuna viongozi ambao wana mapenzi na timu.

"Hii inanipa wasiwasi kuwa tuna matatizo hasa katika kusajili wachezaji, kitu gani ambacho kinawapa TFF kufanya maamuzi mpaka zinapita siku tatu, mbili hii haipendezi.


"Sisi Serikali haiwezekani kuingilia haya masuala ya kimkataba lakini ikishindikana basi tunapeleka Baraza la Michezo Tanzania, (BMT) ikishindikana kabisa wataniletea waziri ndani ya dakika 10 tu nitakuwa nimetoa maamuzi," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Hii kazi wangepewa wajumbe waliowafyelemba akina ninii.... Dakika 3 tu.

    ReplyDelete
  2. Hawa jamaa imekuwa kama ogopa ni heri kama hawajiaminimanbo yasischwe hivo wapewe waamuzi wamalize kwa dakika chavhe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic