KIKOSI cha Yanga leo Agosti 21 kimeendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Septemba 6.
Yanga ilianza mazoezi Agosti 10 na inatumia Uwanja wa Chuo cha Sheria pia inajiaandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa na inaelezwa kuwa inaweza kuwa dhidi ya Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda.
Nyota wake wengi wapya walikuwa ndani ya kikosi ikiwa ni pamoja na Farid Mussa, Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Abdallah Shaibu maarufu kama Ninja, Waziri Junior.
Pia mastaa wengine ni pamoja na Ditram Nchimbi, Lamine Moro, Feisal Salum, Metacha Mnata hawa walikuwa na timu msimu uliopita wa 2019/20.
Mchezo wa Kwanza wa Ligi Kuu Bara kwa Yanga itakuwa Septemba 6 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wanafanya mipango kwa kuzingatia weledi wa kazi.
"Ndani ya wiki ya Wananchi tutaitangaza timu ambayo tutacheza nayo kwani tulikuwa tumetuma maombi sehemu nyingi kupata timu ya kucheza nayo, hata hiyo Rayon Sports tumewatumia pia barua hivyo tutaweka wazi timu tutakayocheza nayo hivi karibuni," amesema.
Simba ondosha mguu atie mwengine
ReplyDelete