September 26, 2020


 FULGENCE Novatus, Kocha Mkuu wa Gwambina FC amesema kuwa kupoteza kwake mechi mbili ndani ya Ligi Kuu Bara kunampa hasira ya kujipanga kupata ushindi wa kwanza ndani ya ligi mbele ya Simba.

Gwambina FC ilianza kuyeyusha pointi tatu ilipomenyana na Biashara United, Uwanja wa Karume Mara kwa kufungwa bao 1-0 kisha iliyeyusha pointi tatu kwa kufungwa bao 1-0 na ina pointi moja iliyopata baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Gwambina.

Leo Septemba 26 ina kibarua cha kumenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku mchezo wa ligi ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.


Huu ni mchezo wa kwanza wa ushindani kukutana na Simba ndani ya ligi kwa kuwa ni msimu wa kwanza wa Gwambina kushiriki ligi baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza.


Novatus amesema:"Ninatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu na ushindani mkubwa ila haina maana kwamba tutawahofia wapinzani wetu ndani ya uwanja.


"Kupoteza kwetu mechi zilizopita ni fundisho kwetu na tunakazi ya kupambana ili kupata pointi tatu kwa kuwa ni kitu ambacho tunahitaji. Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti tutafanya vizuri." 

Miongoni mwa nyota ambao wanatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi ni pamoja na Paul Nonga ingizo jipya kutoka Lipuli ambaye hakuwa na kikosi cha kwanza kwa muda wa wiki tatu akitibu kifundo cha mguu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic