September 26, 2020

 


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amefichua kuwa tatizo kubwa la safu yake ya ushambuliaji ni kushindwa kumalizia nafasi wanazozipata ndani ya uwanja wakiwa wanapambana.

Raia huyo wa Ubelgiji amesema kuwa kwenye mchezo dhidi ya Biashara United ambapo aliwatumia washambuliaji wake Chris Mugalu na Meddie Kagere wakati wakishinda mabao 4-0 tatizo lilikuwa kwenye umaliziaji.

‘Nimegundua tatizo moja kubwa ambalo linaitesa safu yangu ya ushambuliaji ni kwenye umaliziaji wa nafasi ambazo zinatengenezwa ndani ya uwanja. Kwa kugundua tatizo hilo ninalifanyia kazi na ninaamini kwenye mechi zetu zijazo halitakuwepo,” alisema Sven.

Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na vichwa vinne ambavyo ni Chris Mugalu, Meddie Kagere,Charlse Ilanfya na John Bocco ambapo washambuliaji wake watatu wametupia bao mojamoja ndani ya ligi isipokuwa Ilanfya ambaye hajapata nafasi ya kuanza kwenye mechi zote tatu.


Leo Septemba 26 wana kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Gwambina FC iliyotoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini ambao kwa sasa umefungiwa na Bodi ya Ligi mpaka pale utakapofanyiwa maboresho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic